Huduma ya kutibu kwa mbinu za kisasa za radiolojia yaanzishwa MOI (Intervention Radiology)

Madaktari Bingwa wa Radilojia wa MOI wameshirkiana na wenzao kutoka Chuo Kikuu cha Yale marekani, chuo kikuu cha Afya MUHAS, hospitali ya Taifa ya Muhimbi na wengine kutoka hospitali za mikoa wanashiriki katika kambi maalum ya wiki mbili ya huduma ya kibingwa ya uchunguzi wa radilojia (Intervention radiology) ambayo haifanyiki hapa nchini.
Awali wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kufuata huduma hii kutokana na kutokuwepo kwa vifaa na utalaamu wa kufanya huduma hizo ambapo kwa sasa Serikali ya awamu ya tano imeiwezesha taasisi ya MOI kuwa na vifaa vinavyowezesha huduma hiyo kufanyika hapa nchini.
Daktari bingwa wa radiolojia MOI Magda Ahmed amsema kwamba kambi hii ilianza tarehe 23/10/2018 katika kitengo cha radiolojia cha MOI na wagonjwa wamelazwa katika wodi maalum ya kulazwa siku hiyohiyo na kufanyiwa upasuaji siku hiyohiyo‘Sameday Sugery’
“kambi hii itatunufaisha sana kwani toka ianze tunapata mbinu mpya za uchunguzi wa ambazo awali hatukuwa nazo, sasa hivi tuna vifaa vya kutosha hivyo ni muhimu wataalamu kama hawa wakaendelea kuja ili tubadilishane uzoefu kwani wagonjwa wengi wanahitaji huduma hizi lakini hazipo” Alisema Dk Magda.
Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo Dk Rahma Hingora amesema mbinu walizopata zitawazesha kuwahudumia wagonjwa kwa wakati na itawapunguzia adha ya kwenda kutafuta huduma hii nje ya nchi kwani suala hilo limekuwa changamoto kwa wagonjwa na kwa Serikali kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi.
“Ni jambo jema tumejumuika na wenzetu wa Yale marekani, MNH, MUHAS na wengine kutoka hospitali ya Benjamini Mkapa, hapa tunajifunza na pia tunabadilishana uzoefu na mbinu za uchunguzi kwani lengo letu sote ni kuhakikisha mgonjwa anapata huduma bora na kwa wakati popote pale alipo” Alisema Dk Hingora
Taasisi hizi zinashirikiana ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini.