Upasuaji wa Ubongo wa kihistoria wafanyika MOI

Leo upasuaji mkubwa wa kuzibua vivimbe kwenye Ubongo (Celebral aneurysm) umefanyika kwa mara ya kwanza hapa MOI kwa mafanikio makubwa. Upasuaji huo umefanyika kwa masaa 5 kwa kutumia darubini yakisasa ambapo jopo la madaktari bingwa waliofanya upasuaji huo limeongozwa na Profesa Philip Stieg kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani. Upasuaji huo umefanywa kwa mgonjwa aliyepata kiharusi. Awali wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu haya kwa gharama kubwa.