MOI yasini mkataba na Chuo kikuu cha Peking China katika masuala ya tiba

Dar es Salaam, 17/08/2018. TaasisiyaTibayaMifupa Muhimbili (MOI) imesainimkataba waushirikiano Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China. Mkataba huo utajikita katika maeneo ya tiba, utafiti na mafunzo, umesainiwana MkurugenziMtendajiwa MOI Dkt. Respicious Boniface pamoja na Raiswahospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking Prof Hongxia Yu ambapo MOI itanufaika katika kuboresha huduma za kibingwa za daraja la juu (Super specialised services) katika maeneo ya upasuaji wa Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu.
Hafla ya kusaini mkataba huo imeshuhudiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu pamoja na Baloziwa Tanzania nchini China Mh. Balozi Mbelwa Kairuki pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Kambi.
Aidha, hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi nchini China kufanya kikao na Rais wa Hospitali ya kimataifa ya chuo kikuu cha Peking jijini Beijing kuhusiana na kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za tiba za kibingwa hapa nchini.
Hospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking ina uzoefu mkubwa katika matibabu ya Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu ambapo ina vitanda 1800 vyakulaza wagonjwa, ICU vitanda 171, Vyumba vya upasuaji 48 na kwa mwaka inahudumia zaidi ya wagonj wamilioni 14.7