Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

MOI YATANGAZWA KITOVU CHA WELEDI

Author :

Taasisi ya Tiba ya mifupa imetangazwa kitovu cha weledi duniani katika upasuaji wa mfupa mrefu wa paja na wa chini ya goti, hiyo ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji na kwa mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yeyote duniani na hivyo nchi nyingine kuja kujifunza hapa MOI

Date : 30 Jul 2015

MOI YAENDESHA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UPASUAJI WA MIFUPA YA WATOTO

Author :

Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Serikali ya Uturuki imeratibu mafunzo yanayohusisha mbinu mpya za kutibu mifupa ya watoto kwa madaktari wa fani ya tiba ya mifupa ya watoto wa MOI kuanzia tarehe 16/06/2015 mpaka 19/06/2015

Date : 30 Jul 2015

DAKIKA 67 ZATUMIKA KUMUENZI MANDELA WODINI KWA VITENDO

Author :

Jumuiya ya Kimataifa imemuenzi Muasisi wa Taifa la Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela Katika siku yake ya kuzaliwa inayoadhimishwa tarehe 18 July kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika wodi ya Watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji , Mgongo wazi (Hydrocephulus and Spinal Bifida) na Mifupa waliolazwa Wodi A hapa MOI

Date : 30 Jul 2015

MH ZAKIA MEGHJI MWENYEKITI MPYA BODI YA WADHAMINI MOI

Author :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mh Zakia H.Meghji (MB) kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI, uteuzi huu umetokana na bodi ya wadhamini iliyokuwepo kuisha muda wake, uteuzi huo utadumu kwa miaka 3

Date : 07 Sep 2015

MOI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Author :

Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imeshiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kuanzia tarehe 24-28 August 2015 katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam,Maadhimisho hayo yalifunguliwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam CP Suleiman Kova

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano