Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

Posted on 30 Jul 2015

Taasisi ya Tiba ya mifupa imetangazwa kitovu cha weledi duniani katika upasuaji wa mfupa mrefu wa paja na wa chini ya goti, hiyo ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji na kwa mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yeyote duniani na hivyo nchi nyingine kuja kujifunza hapa MOI

Zaidi ya wagonjwa 4800, wamefanyiwa  upasuaji wa mifupa mirefu toka Mwaka 2008 ambapo Taasisi ya MOI ilipoanza kutumia utaalamu wa kutibu mifupa iliyovunjika kwa kuweka vyuma maalum vinavyojulikana kama SIGN NAIL, tiba ambayo inamfanya mgonjwa aweze kupona kwa haraka na aweze kurudi katika hali yake ya kawaida

MOI imetangazwa kuwa kitovu cha weledi na Rais wa Taasisi ya SIGN GROUP INTERNATIONAL ya Marekani Katika mafunzo ya siku 3 ya madaktari bingwa wa mifupa  kutoka nchi mbali mbaili duniani wamekuja hapa MOI kujifunza namna ya kutibu mifupa hiyo mirefu na mingine kama kiuno ,chini ya goti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuweka vyuma inayomwezesha mgojwa kutembea kwa haraka na kurudi katika hali yake ya kawaida

Pamoja na mambo mengine madaktari wa MOI na wengine wa Afrika wamepewa mbinu mpya na madaktari bingwa kutoka marekani  ya kufidia kipande cha mfupa kilichopotea baada ya ajali kwa kuweka mfupa wa bandia na kuunganisha mfupa hivyo kumuondoa mgonjwa katika hatari ya kupoteza kiungo au kiungo kama mkono au mguu kuwa mfupi na kurudi katika hali ya kawaida

Hii ni sehemu ya mkakati wa Taasisi ya MOI na serikali wa kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na MOI inaendelea kuwa kitovu cha weledi katika matibabu ya mifupa, ubongo,mgongo na mishipa ya fahamu, katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.

 

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano