Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

Posted on 30 Jul 2015

Kongamano la kimataifa la Upasuaji wa Ubongo na Mgongo lililofanyika MOI limewanufaisha zaidi ya wagonjwa 30 ambao walitakiwa kwenda nje ya nchi kufuata matibabu na hivyo kufanyiwa Upasuaji hapa MOI kwa kutumia Mbinu Mpya ya kutumia darubini maalumu yani (Brain Navigation)

Pamoja na mambo mengine Mbinu hii inamwezesha daktari kufanya upasuaji kwa kuona kwenye runinga maalumu na hivyo kufuatilia kile anachokofanya kwa umakini na kufika kwenye tatizo bila kuathiri maeneo mengine na hivyo upasuaji kuwa na matokeo bora

Mbinu hii na nyingine zimetolewa katika Kongamano la pili la madaktari wa Upasuaji wa uti wa Mgongo na Ubongo wa Afrika Mashariki na Kati kwa siku 4 kuanzia tarehe 11-15 mwezi May 2015 ambapo Madaktari zaidi ya 100 kutoka kote duniani walishiriki, Kongamano hilo liliratibiwa na Taasisi ya MOI  na Chuo Kikuu cha Cornel cha Marekani

Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dr Othman Kiloloma alisema kutokana na mabadiliko ya Teknolojia duniani ni muhimu wataalamu wakapata mafunzo kama haya ili kuendana na dunia ya kwanza na kuwawezesha madaktari kuwahudumia wagonjwa vizuri zaidi

Aidha, Dr Kiloloma alisema, kutokana na Ongezeko kubwa la ajali limepelekea ongezeko kubwa la majeruhi wanaohitaji upasuaji wa Ubongo na Mgongo hivyo ni Muhimu madaktari wapewe mafunzo ili kuwatia Moyo wale ambao hawajabobea kubobea katika Nyanja hii kwani kuna uhaba mkubwa wa mabingwa wa upasuaji wa Ubongo na Mgongo

Taasisi ya MOI imekuwa ikiendesha makongamano kama haya kutokana na kuwa na Taasisi ya kujifunzia, utafiti ambapo imekua nguzo muhimu katika matibabu ya magonjwa ya Mifupa na Ajali, Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo huduma ambazo hazipatikani katika hospitali nyingine Tanzania.

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano