Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 23 Mar 2015

Posted on 23 Mar 2015

 WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WACHANGIA DAMU MOI

Mwishoni mwa wiki zaidi ya waumini 100 wa dini ya kiislamu kutoka sehemu mbali mbali za mji wa Dar es Salaam chini ya Taasisi ya AKHLAAQ UL ISLAM (Matendo mema ya Kiislamu) waliendesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari kwa ajili ya kuwasadia wagonjwa waliolazwa na wenye mahitaji ya damu

Kutokana na zoezi hilo, kwa siku ya Jumamosi na Jumapili pekee zaidi ya wagonjwa 25 wa dharura na waluiokuwa wodini wakisubiri damu walinufaika kwa kufanyiwa upasuaji baada ya kupata damu

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu kiongozi wa Taasisi hiyo Amir Yahaya alisema Taasisi yao kupitia kitengo chake cha Ustawi wa jamii wamekuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa Damu katika Hospitali mbali mbali hapa Dar es salaam kwani “uchangiaji wa damu ni zawadi kwa wagonjwa wenye uhitaji”

Amir Yahaya aliongeza kwamba Taasisi yao imejipanga kuratibu uchangiaji wa damu mara kwa mara kutokana na kuguswa na changamoto ya ukosefu wa damu na vilevile uchangiaji wa damu ni “thawabu”

Kwa upande wake Msemaji wa MOI Bwana Jumaa T.Almas alishukuru kwa moyo wa upendo na huruma ulioonyeshwa na Jumuiya ya Waislmu kwani ni ishara ya matendo mema na ni mwanzo mpya katika jitihada za kuokoa maisha ya watanzania wengi wanaopoteza maisha kutokana na kukosa damu

Bwana Almasi aliongeza kwamba hivi sasa kuna changamoto kubwa ya uhaba wa damu kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambalo limepelekea ongezeko la wagonjwa wengi wa dharura ambao wengi waowanahitaji damu ili waweze kufanyiwa upasuaji na hivyo kuiomba jamii kwa ujumla kuiga mfano mzuri ulioonyeshwa na AKHLAAQ UL ISLAM

Baadhi ya wagonjwa wamekua wakipoteza maisha kutokana na kukosa damu kutokana na uhaba wa damu kutoka Benki ya Damu (Damu Salama) hivyo uchangiaji wa hiari unaweza kuwa sehemu ya suluhisho na kuokoa maisha ya watanzania hasa wale waliopata ajali na kuhitaji damu ili kufanyiwa upasuaji.

Kutokana na zoezi hilo la uchangiaji wa damu kuwa na mafanikio makubwa Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Taasisi ya AKHLAAQ zimelifanya zoezi hilo kuwa endelevu likihusisha wanajamii ambapo wafanyakazi wa MOI wameunga mkono kwa kuchangia damu ili kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu. 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano